ZIARA YA NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS -TAMISEMI

ZIARA YA NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS -TAMISEMI

Tarehe 8 mpaka 12 Disemba, Mradi wa Kukabiliana na athari na Changamoto za Mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianchi ulipata fursa ya kutembelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Joseph George Kakunda.

Mradi wa Kukabiliana na Athari na Changamoto za Mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianchi unatekelezwa katika wilaya tatu, Longido, Monduli na Ngorongoro. Mradi huu unatekelezwa na  ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Chuo cha Mipango (IRDP), Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) na HakiKazi Catalyst.Mradi huu umefadhiliwa na Serikali ya Uingeleza kupitia shirika lake la maendeleo (DFID)pamoja na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF).

Mheshimiwa Naibu Waziri, OR-TAMISEMI, alipata fursa ya kutekutembelea miradi saba (7) kati ya miradi thelathini na nne (34) iliyofadhiliwa na mradi huu. Miradi iliyotembelewa ni ifuatayo;

Mradi wa..

  1. Ujenzi wa tenki la maji, pamoja na kituo cha kuchotea maji na kituo cha mifugo kunywea maji kijiji cha Eorendeke kata ya Kimokowa – Longido
  2. Ukarabati wa mfumo wa maji wa Engaruka kijiji cha Irerenden, kata ya Engaruka – Monduli
  • Ukabarati wa Lambo la Olobo, Ujenzi wa eneo la mifugo kunywa maji na kituo cha kuchotea maji – Ngorongoro
  1. Ukarabati wa chanzo cha maji, kuweka uzio katika chanzo cha maji, kujenga eneo la mifugo kunywa maji na kituo cha kuchotea maji, Wasso – Ngorongoro
  2. Ukarabati wa lambo la Olbalbal – Ngorongoro
  3. Ujenzi wa maabara ya utafiti wa magonjwa ya mifugo – Ngorongoro
  • Kuzungushia uzio vituo 6 vya Hali ya hewa – Ngorongoro

Mradi wa Kukabiliana na Athari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi haukuwa tu mradi pekee uliotembelewa. Katika ziara yake, Naibu Waziri alifanikiwa kutembelea na kukagua miradi mingine ya jamii inayohusu shule, maji na ujenzi.

Kwa niaba ya wadau wote wa Mradi wa Kukabiliana na Athari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi tunasema ASANTE kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Joseph George Kakunda (Mb).

 

 

 

Leave a Reply